Thursday, December 1, 2011

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA IGUNGA (KWENYE KAMPENI) UPANDE WA CHADEMA


Taswira Za Uzinduzi Wa Kampeni Za Chadema igungaAnaitwa Joseph Kashinye, Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga. “Ninashughulikia kupata mtandao wa uhakika. Leo siku haitoisha, nitakuwa nimepata suluhu la tatizo la Mtandao. Nitawaporomoshea kila kinachojiri huku. Asubuhi hii nimebahatisha kuingiza picha hiyo kwa taabu, imenichukua saa mbili kuingiza picha moja!  Pichani Kashindye alikuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa Igunga katika uzinduzi wa kampeni

.


Mabango yenye ujumbe tofauti katika mkutano wa CHADEMA jana

.Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa akihutubia mjini Igunga jana katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni hapa.
Dr Slaaa alisema CCM hawana sababu ya kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ile kwani kwa kipindi cha miaka 50 imeshindwa kumkomboa Mtanzania katika lindi la umaskini.
Aliongeza kuseam kuwa CCM wanachokizinatia ni kutumia kila mbinu ili kushinda chaguzi na kushika dola ikiwa hawana malengo na mikakati madhubuti ya kumkomboa Mtanzania. Aliwaasa wana Igunga kumchagua Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye, ili awe mwakilishi wao kwani ni mtu makini anaetoka katika chama makini.Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la Igunga.
Mbowe alisema kuwa wana Igunga mungu amewapa bahati kubwa ya ufaya uchaguzi muda ,fupi  baada ya uchaguzi mkuu. Hivyo waitumie bahati hiyo wa kufanya mabadiliko.
CCM haistaili kurudishwa tena madarakani jimboi hapa, kwani kuna masuala mengi ya msingi yanayohusiana na maendeleo ya wananchi CC imeshindwa kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka 50Ilifika zamu ya Mgombea wa Ubunge jimboni hapa kwa Tiketi ya Chadema, Mwalimu, Mkaguzi wa Elimu, Joseph Lashindye.Kashindye alisema kuwa wana Igunga wtarajie mabadiliko ya haraka katika maendeleo.
Yeye ameamua kwa makusudi kuacha ualimu na kuingia katika ulingO wa siasa. Amefanya kama Mwalimu Nyerere alivyofanya kwani Mwalimu Nyerere, aliaacha ualimu na kujiunga na TANU, matokea ya uamuzi huo wa mwalimu hakuna Mtanzania asiyeyaju.
Na yeye alisema kuwa endapo wana-Igunga watamapa ridhaa ya kuwa mwakilishi atasimamia kwa nguvu zake zote misingi ya utu, uchapakazi na atahakikisha anaziba mianya yote ya rushwa katika halmashauri ya wilaya, ili fedha zinazotafunwa na wajanja, zifanye kazi iliyokusudiwa ya kuwaletea maendeleo wana- Igunga.Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwahutubia wananchi wa jimbo la Igunga jana jioni katikauzinduzi wa kampeni za ubunge jimboni humo.Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.
Mbunge wa Mbeya Mjini-Chadema Mheshimiwa Joseph Mbilinyi aka Mr II(Sugu)akiwa amezungukiwa na mashabiki wa chama hicho igunga muda mfupi baada ya Chadema kuzindua Kampeni zake za Uchaguzi Mdogo.Kutoka kulia ni katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho na mbunge wa jimbo la Hai wakielekea kwenye mkutano

.


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la Igunga

.


Sehemu Kubwa ya Umati wa Wanachama Wa Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo(Chadema)akielekea kwneye uzinduzi rasmi wa kampeni za Kuwania jimbo hiloMabango yalikuwa ni mengi lakini pia jeshi la polisi lilihakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha
KUSHINDWA KWA CHADEMA IGUNGA KUNATUPATIA SOMO NA PICHA IPI?
 

UCHAGUZI mdogo wa Igunga umekwisha na ktuachia mafunzo mengi.  Kubwa kabisa ni kwamba, wananchi wanahitaji mabadiliko kwa kila kitu katika maisha yao na kubwa zaidi linabakia kuwa nani atakuwa kiongozi wa mabadiliko yao.

Dalili zote zinaonekana zikielekea upande wa mabadiliko ya kweli japo pole pole na mabadiliko haya siyo ya kichama ni ya watu binafsi mmoja mmoja, ni mabadiliko ya fikra kwanza, kabla ya mabadiliko ya kura.
Hivi ni nani anaamini kuwa leo hii jimbo kama la Igunga ambalo lilikuwa likiaminika kuwa ni ngome tena ngome sugu ya CCM, leo wanavunja ngome yao na kukimbilia kambi ya upinzani.

Kwa mtu wa kawaida na mwenye mawazo ya kawaida tu lazima ajiulize kuwa je, hivi ni kweli kwamba mikutano ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja imewabadilisha kiasi hicho au ni mabadiliko yaliyokuwamo ndani?
Mwingine atajiuliza swali, hivi yale maneno yaliyokuwa yakivuma wakati fulani kuwa hiyo ni ngome ya chama tawala yalikuwa ya kweli au yalikuwa ya kuokoteza tuu?

Ukifanya tathmini kwa kina, utabaini kuwa kuna jambo linatokea kwa Watanzania ambalo ni kukata tamaa kunakosababisha watu watake mabadiliko na mabadiliko yamekosa mwongozaji na sasa wanaangukia kwa chama wanachodhani kitawapeleka katika mabadiliko hayo.
Hakuna atakayaweza kuzuia mabadiliko haya, siyo CCM wala serikali yake. Yawezekana CCM ndiyo ikawa chanzo cha mabadiliko hayo au yawezekana pia Chadema au chama kingine ikawa ndiyo kichocheo na kiongozi wa mabadiliko na haitashangaza.

Nimefuatilia kwa makini matokeo ya uchaguzi ndogo wa Igunga wa Oktoba 2, CCM kimeshinda kwa kura 26,484 huku Chadema  kikivuna kura 23,260 kutokea ziro ndani ya mwaka mmoja. Chadema kilishindwa kwa tofauti ya kura 3,224 huku kura 1,185 zikiharibika.
Kwa chama ambacho uchaguzi uliopita kilikuwa hakishikiki Igunga, yaani CCM ambacho kilikuwa kikipita bila ya kupingwa hii ni ishara ya kwanza kubwa ya upepo mbaya kuvuma kwao. Ni kwamba bundi katua kwenye paa la nyumba yao!

Chadema wameshindana na vikwazo vingi katika njia ya kufikia hapo ilipofika ikiwamo kushindana na Serikali nzima, serikali ya wastaafu na vikosi vya dola la taifa hili, ni ishara ya upepo wa mabadiliko kuvuma.

Hali hiyo imeipa tabu sana CCM. Kutokana na wnanchi wa Igunga kukata tamaa huko kumeibua chuki dhidi ya chama hicho na viongozi wake. Ilikuwakabiliana na hilo chama kilikuwa kinatumia mtaji wa kuwatisha kwa mbinu mbalimbali.
Kuna wakati watu walifikiria kwamba, Chadema kingeshinda Igunga. Walifikiria kwamba , baada ya CCM kupoteza imani ya wananchi wataendelea kuonyesha kinavyoporomoka baada ya kuondoka kwa Rostam Aziz.

Kwa CCM kuachia au kupoteza ushindi upinzani wakati wao kama chama, walitaka kuwaonyesha wananchi kwamba kuondoka kwa Rostam si pigo la chama na chama kitaendelea kuwatumikia wananchi na si Magamba.
Kwa muda wote CCM wamekuwa wakitumia vyombo vya dola ambavyo wamerithi kutoka CCM ya chama kimoja toka wajumbe wa nyumba kumi, wamekuwa wakitumia wajumbe wa Halmashauri za miji.

Wamewatumia walimu na wakuu wa wilaya ili kuonyesha nguvu ya chama kiutawala, nguvu ambayo vyama vya upinzani havina. Kwa kila hali, utaweza vipi kushindana na chama kilichoshika mpini?.

Leo hii tunashuhudia kinachotokea Igunga na kujifunza kumbe Chadema kina udhaifu katika mkakati wa kuimarisha chama kwa maana ya kujenga mtandao. Mfano halisi ni kwamba, chama hicho hakikuwapo kabisa kabla ya kuanza kampeni, lakini kikawazoa wana-Igunga waliojikatia tamaa ndani ya wiki chache.

Ninavyoona mimi Chadema kinapaswa kutumia vema umaarufu wake kwa watu kwa kujenga mtandao, si kuishia kuruka kwa helikopta pekee wakati wa uchaguzi, kubabaishwa na wingi wa watu kwenye mikutano yake na hatimaye kutokuwa na uhakika wa kura kinazoweza kupata.

 

Kampeni za Chadema Igunga katika picha
Ummati ukiandamana kwenye kampeni za CHADEMA Jimboni Igunga.
KAMPENI za kugombea ubunge Jimbo la Igunga zinaendelea huku vyama vyenye upinzani mkali katika jimbo hilo vya CHADEMA, CCM na CUF vikiendelea kunadi wagombea wao kwa mbwembwe.
Jimbo hilo limeachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa CCM Jimbo la Igunga, Rostam aziz baada ya kujiuzulu kwa shinikizo kutoka ndani ya CCM. Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionesha mikutano ya CHADEMA


Mikutano ya CHADEMA IgungaKutoka kulia ni katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho na mbunge wa jimbo la Hai wakielekea kwenye mkutano

 

Chadema Igunga: Pepople's PowerrrrrrrMwenyekiti wa Chama cha Chadema Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Nkinga wa kuwania kiti cha Ubunge cha jimbo la Igunga baada ya kuwasili na Helkopta

               TAANZIA YA KIFO KWENYE UCHAGUZI IGUNGA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Kichama wa Kinondoni Kanda Maalumu Dar es salaam kinasikitika kutangaza kifo cha mwanachama Mbwana Masoud kilichotokea wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga. Marehemu Mbwana Masoud alikuwa ni mmoja wa wanachama walijitolea kusafiri kwenda Igunga kwa ajili ya kuwa wakala kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 2 Oktoba 2011. Marehemu Mbwana Masoud alitoweka katika mazingira ya kutatanisha wilayani Igunga tarehe 2 Oktoba 2011.
Baada ya jitihada za viongozi wa chama kumtafuta marehemu kushindikana Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika (Mb) alitoa taarifa polisi tarehe 3 Oktoba 2011 na kufungua jalada RB/748/2011.
Tarehe 9 Oktoba 2011 wananchi wilayani Igunga walikuta mwili wa marehemu ukiwa porini katika eneo ambalo linajulikana zaidi kama msitu wa magereza. Taarifa ilitolewa na wananchi kwa diwani wa kata ya Igunga Vicent Kamanga (CHADEMA) ambaye alifika katika eneo hilo na baadaye maafisa wa polisi walifika na kupeleka mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Tarehe 9 Oktoba 2011 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alitembelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Kwa Jongo Kata ya Makurumla kuifariji familia ya marehemu na kukubaliana na ndugu wa marehemu kutuma wawakilishi wa chama na familia kwenda Igunga kuhakiki mwili uliopatikana.
Tarehe 10 Oktoba 2011 wawakilishi wa familia wakiwa pamoja na Katibu Mwenezi wa Chama Wilaya ya Ubungo Ali Makwilo walishuhudia mwili husika na kuthibitisha kuwa ni wa marehemu Mbwana Masoud.
Leo Tarehe 11 Oktoba 2011 mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari (post mortem) kuweza kubaini chanzo cha kifo na ripoti wamepatiwa jeshi la polisi. Hata hivyo, mazingira ya kupatikana kwa mwili wa marehemu yanaashiria marehemu  Mbwana Masoud aliuwawa.
Kutokana na hali ya mwili wa marehemu, maziko yatafanyika leo tarehe 11 Oktoba 2011 alasiri katika kata ya Igunga yakihusisha wawakilishi wa familia ya marehemu, viongozi wa chama, wanachama na wananchi wa maeneo husika kwa ujumla.
Viongozi waliopo kwenye maziko hayo ni pamoja na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tabora, Halfan Athumani, Diwani wa Kata ya Igunga Vicent Kamanga na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga kupitia CHADEMA, Joseph Kashindye.
Hitma ya Marehemu itafanyika hapa Dar es salaam nyumbani kwa marehemu Mtaa wa kwa Jongo Kata ya Makurumla tarehe 13 Oktoba 2011 saa 7 mchana baada ya swala ya adhuhuri na itahudhuriwa na viongozi waaandamizi wa chama ngazi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Chama kitaendelea kuwa pamoja kwa hali na mali na wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kinavitaka vyombo vya dola kuharakisha uchunguzi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wahusika. Marehemu amekufa akiwa katika safari ya kulinda haki na kutetea demokrasia na maendeleo; apumzike kwa amani.
MAUAJI YA KUSIKITISHA NA YA KINYAMA YANAYOTISHIA AMANI YA MTANZANIA
NI wakati wa kulaani siasa za chuki na uhasama, kwani zimesababisha umwagaji damu maeneo mengi barani Afrika na dunia kwa jumla, Tanzania mambo yameharibika na hivi ndivyo wakala wa Chadema alivyouawa Igunga.

Masoud Mbwana, baba wa mtoto mmoja, hivi sasa amelala kwenye mwanandani wa kaburi, chanzo kikidaiwa ni mchakato wa uchaguzi mdogo, uliochukuwa nafasi Jimbo la Igunga Oktoba Pili, 2011

.

 
Mazishi ya Masoud Mbwana.
Mbwana, kada wa Chadema, alichukuliwa Dar es Salaam na chama chake kwenda kusaidia shughuli za kampeni na uchaguzi, mwisho wa safari hiyo ikawa ndiyo sababu ya kifo chake.

Wakala huyo, alikutwa ameuawa porini, macho yamenyofolewa na shingo limevunjwa.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Ally Hassan Matumla, uchaguzi Igunga ulifanyika Oktoba Pili, mwaka huu, siku iliyofuata walipokea taarifa kutoka kwa vijana wengine wa Chadema kuwa Mbwana haonekani.

Katika mahojiano na mwandishi wetu yaliyofanyika Mtaa wa Jongo, Makurumula, Magomeni, Dar, Matumla alisema kuwa kazi ya kumtafuta Mbwana ilianza kufanywa na vijana wa Chadema ambao walikuwa wakiijulisha familia hatua kwa hatua. 
Mwili wa Masoud Mbwana ukiwa umetupwa porini.
 “Siku iliyofuata tukapewa taarifa kwamba kuna mtu amegongwa na gari. Ikabidi familia initeue kwenda Igunga kufuatilia. Niliondoka Dar Oktoba 6 na kufika Igunga siku hiyo hiyo saa 10:45 alasiri.

“Nilifika ofisi za Chadema, nikaongozana na viongozi hadi polisi. Hata hivyo, yule aliyegongwa na gari hakuwa yeye. Jumapili (Oktoba 9), saa 8 mchana, tulipata taarifa kuwa kuna maiti ameokotwa porini, karibu na Gereza la Igunga.

“Oktoba 10, tuliongozana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kwenda chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Wilaya ya Igunga, hapo ndipo tulifanikiwa kumkuta akiwa na majeraha mengi.

“Mwili wa mdogo wangu  ulikuwa na majeraha kisogoni, inaonekana alipigwa, macho yalitobolewa, mikono na miguu ilikuwa na majeraha mengi kuonesha aliburuzwa. Polisi walichukua maelezo yetu na kuuzika mwili wake kwa sababu ulikuwa umeharibika mno,” alisema Matumla.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa amelaani mauaji hayo na kuitaka serikali ifanye uchunguzi makini, kuwapata watuhumiwa.


 
Mwili wa Masoud baada ya kutolewa porini.

Slaa alisema: “Nawaomba wana familia muwe watulivu, ni msiba mzito lakini tungoje uchunguzi utakaofanikisha kuwapata watuhumiwa.”

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliliambia gazeti hili kuwa chama chake kinalaani mauaji hayo, hivyo kinawapa pole familia na Chadema kwa sababu Mbwana alikuwa wakala wa chama hicho.
“Kwa kipindi hiki, tuache vyombo vya dola vifanye uchunguzi wake,” alisema Nape.

Uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, ulitawaliwa na matukio mbalimbali ya vurugu, ikiwemo nyumba kuchomwa moto, mwingine alimwagiwa tindikali na mpaka risasi zilirindima katika vurugu za wafuasi wa CCM na Chadema.


 
Masoud Mbwana enzi za uhai wake.

Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea wa CCM, Dalaly Peter Kafumu alishinda akifuatiwa kwa karibu na Joseph Kashindye wa Chadema.

PICHA NA GROBALPUBLISHERS TANZANIA
.

No comments:

Post a Comment