Wednesday, December 21, 2011

KANNALI MUAMMAR GHADAFFI; NI VIZURI NIKAACHA WOSIA KABLA YA KUFA ILI HATA VIZAZI VIJAVYO VIJIFUNZE KUPINGA UONEVU KWA MANUFAA YA JAMII, TAIFA NA ULIMWENGU KIUJUMLA


SINTA ACHA KUPIGANIA NCHI YANGU  HADI KIFO CHANGU
WOSIA WA GHADAFI KABLA YAKIFO CHAKE KWA WANALIBYAKanali Muammar Gaddafi.
 King Herrysson Dawsson na Mashirika ya Habari
SIKU chache baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, bado kuna mitazamo tofauti kuhusu tukio hilo huku wosia aliouacha ukiwatoa watu machozi, Ijumaa Wikienda linauanika.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa, wosia huo uliosambazwa na waliokuwa wakimuunga mkono Kanali Gaddafi umejaa ujasiri, msimamo wa ajabu na utabiri wa aina ya kifo chake.

WOSIA WASISITIZA MAPAMBANO BILA KUJALI KIFO
Pia wosia huo uliwatia moyo wafuasi wake kuendelea kupambana bila kujali kama yeye yuko hai au kafa, hivyo kuuawa kwake inasadikiwa kuwa ndiyo mwanzo wa chuki na kutafutana ili kulipa kisasi.

Wosia huo uliotafsiriwa kutoka katika lugha ya Kiarabu kwenda Kiingereza unaweka wazi kuwa Kanali Gaddafi alichagua kupigana kiume hadi nukta ya mwisho ya uhai wake na kufia katika ardhi ya Libya.

Ulieleza kuwa kukimbilia uhamishoni nje ya nchi yake kilikuwa ni kitendo cha kujidhalilisha, kisichokuwa na heshima pamoja na kwamba alishapata ahadi za ulinzi.

HUU NDIYO WOSIA WENYEWE
Katika tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili, wosia huo ulisomeka:
“Hii ni hiyari yangu. Mimi Muammar bin Mohammad bin Abdussalam bin Humayd bin Abu Manyar bin Humayd bin Nayil al Fuhsi Gaddafi, ninaapa kwamba hakuna Mungu mwingine zaidi ya Allah na Muhammad ni Mtume wake, amani ipo kwake. Ninaahidi nitakufa nikiwa Muislam.

ALIJUA ATAUAWA
“Najua siku siyo nyingi nitauawa, nawaomba mnizike nikiwa nimetapakaa damu zangu kwa mujibu wa taratibu za Kiislam, nikiwa na mavazi nitakayokuwa nimevaa wakati kifo changu kikitokea, bila mwili wangu kuoshwa.

ALITAKA AZIKWE HAPA, MKE NA FAMILIA WALINDWE
“Nizikwe katika makaburi ya Sirte, (Benghazi, Libya) jirani na familia na jamaa zangu.
“Nitapenda kwamba familia yangu, hasa wanawake na watoto, watunzwe vyema baada ya kifo changu.

“Watu wa Libya wana wajibu wa kulinda sifa, mafanikio, historia na heshima ya waasisi na mashujaa wa taifa lao.
“Walibya hawatakiwi kupuuza kujitapa na lazima wawe watu huru wa kuthaminiwa.

UJASIRI
“Ninawataka wale wanaoniunga mkono kuendelea kupambana, kuwakabili wote wanaosimama kutoka nje dhidi ya Libya, leo, kesho na siku zote. Msikubali hata siku moja kuuza utu wenu kwa wageni.

FUNZO
“Hata kama hatutashinda mapema, tutatoa funzo kwa vizazi vyetu vijavyo, kwamba kuchagua kulinda utaifa ni heshima na kuliuza ni uasi mkubwa ambao historia haitausahau milele, pamoja na juhudi za wengine kuwaeleza kinyume cha hayo”.

TAFSIRI NYINGINE
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo ya kisiasa barani Afrika, Kanali Gaddafi na mwanaye Mutassim walikuwa na udhaifu wao, lakini hawakustahili kifo cha ‘sampuli’ walichokutana nacho.

Kanali Gaddafi anaelezewa kuwa ni aina ya viongozi wa Afrika wenye misimamo mikali kama ilivyo kwa Nelson Mandela na Robert Mugabe.

No comments:

Post a Comment