Tuesday, December 20, 2011

MAFURIKO MBEYA , MWANZA NA DAR ES SALAAM

        

MAFURIKO UWANJA WA NDEGE MWANZA YASABABISHA UWANJA KUFUNGWA KWA MUDA

Mafuriko yawatesa wakazi wa Kiseke, ilemela MwanzaRC, RPC Dar watembelea eneo la mafuriko Sinza na Jangwani


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadik Mecky Sadik, akionesha sehemu iliyoharibiwa na mafuriko, alipowatembelea wakazi wa Sinza kujua athari za mafuriko hayo Dar es Salaam. Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda.
 y
 Kamanda wa Polisi Kanda Maaluma Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova, akionesha moja ya nyumba zilizoko ndani ya maji, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Jijini leo. Watu watatu wamelipotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko hayo.
Watoto wanaoishi eneo la Jangwani wakiwa wamehifadhiwa kwenye kituo cha Daladala, kando ya Barabara ya Morogoro, baada kuzikimbia nyumba zao, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha Jijini Dar es Salaaam na kusababisha mafuriko

Wakazi wa Jiji wakiwa juu ya daraja la Jangwani, kukiangalia vitu mbalimbali vilivyosombwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko.

Mshikemshike wa mafuriko Dar

 Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamekubwa na mafuriko, baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha baadhi ya nyumba kujaa maji na watu kukosa makazi kama inavyoonesha katika picha hizi.Polisi Dar wajipanga kuokoa waliokwama kwa mafuriko

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi, wakiwa katika eneo la tukio Dar es Salaam, kuwalinda wakazi wa eneo la Jangwani waliokumbwa na mafuriko leo

Jiji la Dar lakumbwa na mafuriko

Mvua yasababisha  vifo MbeyaNo comments:

Post a Comment