SINTA ACHA
KUPIGANIA NCHI YANGU HADI KIFO CHANGU
WOSIA WA GHADAFI KABLA YAKIFO CHAKE KWA WANALIBYA
Kanali Muammar Gaddafi.
King Herrysson Dawsson na Mashirika ya Habari
SIKU
chache baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar
Gaddafi, bado kuna mitazamo tofauti kuhusu tukio hilo huku wosia
aliouacha ukiwatoa watu machozi, Ijumaa Wikienda linauanika.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa, wosia huo
uliosambazwa na waliokuwa wakimuunga mkono Kanali Gaddafi umejaa
ujasiri, msimamo wa ajabu na utabiri wa aina ya kifo chake.
WOSIA WASISITIZA MAPAMBANO BILA KUJALI KIFO
Pia
wosia huo uliwatia moyo wafuasi wake kuendelea kupambana bila kujali
kama yeye yuko hai au kafa, hivyo kuuawa kwake inasadikiwa kuwa ndiyo
mwanzo wa chuki na kutafutana ili kulipa kisasi.
Wosia huo
uliotafsiriwa kutoka katika lugha ya Kiarabu kwenda Kiingereza unaweka
wazi kuwa Kanali Gaddafi alichagua kupigana kiume hadi nukta ya mwisho
ya uhai wake na kufia katika ardhi ya Libya.
Ulieleza kuwa
kukimbilia uhamishoni nje ya nchi yake kilikuwa ni kitendo cha
kujidhalilisha, kisichokuwa na heshima pamoja na kwamba alishapata ahadi
za ulinzi.
HUU NDIYO WOSIA WENYEWE
Katika tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili, wosia huo ulisomeka:
“Hii
ni hiyari yangu. Mimi Muammar bin Mohammad bin Abdussalam bin Humayd
bin Abu Manyar bin Humayd bin Nayil al Fuhsi Gaddafi, ninaapa kwamba
hakuna Mungu mwingine zaidi ya Allah na Muhammad ni Mtume wake, amani
ipo kwake. Ninaahidi nitakufa nikiwa Muislam.

ALIJUA ATAUAWA
“Najua
siku siyo nyingi nitauawa, nawaomba mnizike nikiwa nimetapakaa damu
zangu kwa mujibu wa taratibu za Kiislam, nikiwa na mavazi nitakayokuwa
nimevaa wakati kifo changu kikitokea, bila mwili wangu kuoshwa.
ALITAKA AZIKWE HAPA, MKE NA FAMILIA WALINDWE
“Nizikwe katika makaburi ya Sirte, (Benghazi, Libya) jirani na familia na jamaa zangu.
“Nitapenda kwamba familia yangu, hasa wanawake na watoto, watunzwe vyema baada ya kifo changu.
“Watu wa Libya wana wajibu wa kulinda sifa, mafanikio, historia na heshima ya waasisi na mashujaa wa taifa lao.
“Walibya hawatakiwi kupuuza kujitapa na lazima wawe watu huru wa kuthaminiwa.
UJASIRI
“Ninawataka
wale wanaoniunga mkono kuendelea kupambana, kuwakabili wote wanaosimama
kutoka nje dhidi ya Libya, leo, kesho na siku zote. Msikubali hata siku
moja kuuza utu wenu kwa wageni.
FUNZO
“Hata kama
hatutashinda mapema, tutatoa funzo kwa vizazi vyetu vijavyo, kwamba
kuchagua kulinda utaifa ni heshima na kuliuza ni uasi mkubwa ambao
historia haitausahau milele, pamoja na juhudi za wengine kuwaeleza
kinyume cha hayo”.
TAFSIRI NYINGINE
Kwa mujibu wa wachambuzi
wa mambo ya kisiasa barani Afrika, Kanali Gaddafi na mwanaye Mutassim
walikuwa na udhaifu wao, lakini hawakustahili kifo cha ‘sampuli’
walichokutana nacho.
Kanali Gaddafi anaelezewa kuwa ni aina ya
viongozi wa Afrika wenye misimamo mikali kama ilivyo kwa Nelson Mandela
na Robert Mugabe.