KING HERRYSSON
DAWSSON
Mwanaume wa nchini Marekani maarufu kama 'Half Man' ambaye maisha yake yote amekuwa akiishi akiwa na nusu ya mwili wake tu kuanzia kiunoni ametamba kuwa yeye ndiyo baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na mchumba wake ingawa baadhi ya watu hawaamini kama kweli mtoto ni wake wakidai atakuwa kabambikiwa mtoto.
Kenny Easterday mwanaume wa nchini Marekani mwenye umri wa miaka 35 ambaye ana nusu mwili kuanzia kiunoni, anasubiria majibu ya DNA ili kuwathibitishia watu kuwa yeye ndio baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na mpenzi wake Nicky.
Katika documentary mpya itakayorushwa hewani leo kwenye televisheni ya Marekani, Kenny mkazi wa West Virginia anasema kuwa yeye ndiye baba wa mtoto Desiree aliyezaa na mpenzi wake Nicky,33 miaka saba iliyopita.
"Watu wanataka kujua kama Kenny ana sehemu za siri", alisema Nicky katika documentary hiyo itakayorushwa hewani na televisheni ya The Learning Channel (TLC).
"Tunafanya mapenzi kama watu wengine, Kenny ana sehemu za siri kama mwanaume mwingine", aliongeza Nicky.
Kenny alizaliwa akiwa na ugonjwa unaowapata watu wachache sana duniani unaoitwa sacral agenesis ambao huzuia uti wa mgongo kukua kama kawaida.
Madaktari walilazimika kuikata miguu yake miwili iliyojipinda iliyojichomoza kidogo chini ya kiuno chake na kisha kuuchukua mfupa wa ugoko wake na kuutumia kuurefusha uti wa mgongo wake.
Kenny ambaye kutembea kwake ni kwa kutumia mikono anasema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kupata mtoto.
"Nataka niwe na mtoto atakayelibeba jina langu ambaye ataweza kusimama mbele ya watu na kusema 'HUYU NDIYO BABA YANGU'", alisema Kenny.
No comments:
Post a Comment