BAADA YA MASOKO MAWILI KUUNGUA MBEYA, HAYA NDIYO YANAYOENDELEA
Watoto wakitafuta sarafu eneo lilipoungua soko la Sido Mwanjelwa Mbeya juzi.
Ujenzi ukiendelea eneo lilioungua soko la Sido Mwanjelwa Mbeya.
Baada ya kuunguliwa akina mama wanaendelea kujitafutua riziki pambeni kidogo mwa soko hilo
Chadema ilipotua eneo la ajali ya Mwanjelwa baada ya siku moja moto kuzimwa.
Hatimaye siasa zikandelea kata ya majengo Jijini Mbeya. PICHA KUTOKA MTANDAONI
Usiku
wa kuamkia leo huko jijini Mbeya,Moto ambao haukufahamika chanzo chake
uliteketeza soko dogo lililopo maeneo ya Forest ya zamani karibu na Chuo
kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu huria matawi ya Jijini Mbeya na
kusababisha mabada kadhaa kuteketea kwa moto ambao uliwahiwa na kikosi
cha zima moto cha mkoa wa Mbeya.
Mdau
alietuletea picha hizi ambaye alifika eneo la tukio mapema leo asubuhi
na kukuta moto umefanikiwa kuzimwa katika vibanda hivyo vilivyokuwepo
sokoni hapo na kutuletea taswira hizi za mabaki ya mabanda yaliyoungua
moto katika soko hilo yakiendelea kufuka moshi.
Mashuhuda
waliokuwepo maeneo ya jirani na soko hilo walisema Moto huo ulianza
majira ya saa 9:00 kamili usiku na muda si mrefu taarifa ziliwafikia
kikosi cha Zimamoto na wao walifika eneo la tukio dakika 10 baadae na
kufanikiwa kuuzima moto huo bila hata ya maigizo yao ya kila siku ya
kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji au kuharibika kwa gari wakati
wakiwa kwenye tukio.maswali
mengi sana yamekuwa yakiulizwa hivi sasa Jijini Mbeya juu ya majanga ya
moto katika masoko ya Mbeya kila siku na kwanini tahadhari
hazichukuliwi mapema na wakati hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa
mara??
No comments:
Post a Comment