Tuesday, April 10, 2012

MAJONZI YATAWALA DAR VOIONGOZI WA KISIASA KUFURIKA MSIBANI


Monday, April 9, 2012

Mama Salma Kikwete ahani Msiba wa Steven Kanumba

 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Msanii nguli wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba aliefariki Dunia siku mbili zilizopita nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Urambo Magharibi,Mh. Athuman Juma Kapuya akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Msanii nguli wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba aliefariki Dunia siku mbili zilizopita nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam.
 Mkongwe wa Muziki nchini,King Kikii akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Msanii nguli wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba aliefariki Dunia siku mbili zilizopita nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam.
 Mdau Iman Madega akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Msanii nguli wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba aliefariki Dunia siku mbili zilizopita nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akikumbatiana na Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba wakati alipofika nyumbani hapo kwa ajili ya kuhani msiba huo,jioni ya leo.
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimfariji Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba,Nyumbani kwa Marehemu,Sinza Vatican jijini Dar jioni ya leo.Kushoto ni Dada wa Marehemu Steven Kanumba.
 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni,Dkt. Fenella Mukangara wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Steven Kanumba kwa kuhani Msiba huo.Kushoto ni Mama Mzazi wa Steven Kanumba.
 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Waombolezaji wa Msiba wa Marehemu Steven Kanumba jioni hii alipofika kuhani msiba huo.
 Mama Mzazi wa Steven Kanumba.
 
 Mama Salma Kikwete akizungumza na Wasanii wa Bongo Movie jioni ya leo.

Uzinduzi wa Miss Tabata 2012 wafana vilivyo

 Warembo wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jana.
 Warembo wakicheza Show maalum ya utambulisho wao. Goma la Don’t Take My Number ndo liliwaongoza.
Warembo wa wanaoshiriki shindano la kumsakama Malkia wa Tabata 2012 wakipozi mbele ya mashabiki wa burudani ya urembo jijini Dar es Salaam waliohudhuria uzinduzi wa shindano hilo la Urembo katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jana.
 Washiriki wa Shindano la Miss Ukonga 2012 ndio waliowasindikiza majirani zao wa Tabata.
 Mpiga drams wa Twanga Pepeta Martin Kibosho akifanya vitu vyake jukwaani.
 Mwimbaji mkongwe asiyechoka wala kuzeeka, Mumin Mwijuma akikamua na kundi lake la Twanga Pepeta.
 Wanenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta wakishambulia Jukwaa vilivyo.
 Shabiki mkubwa wa Twanga, Tomm Chilala akiyarudi magoma na mdau mwenzake.
 Ilikuwa ni mshike  Mshike kwa show za kufa mtu hakuna kukaa.
Wadau wa Burudani na Urembo wakifatilia burudani na uzinduzi ho ulioletwa na Bob Interteinment na kudhaminiwa na Konyagi na Dodoma Wine.
 Mzee Mzima Salum Simba (MC) machachari akiwa na my wife wake.
 Wadau wakubwa wa masuala ya urembo na Burudani kwa ujumla walikuwepo ukumbini. Pia walitumia fursa hiyo kusheherekea Pasaka.
 Jopo la waandaaaji wa Shindano la Miss Chan'gombe walikuwepo kuangalia vitisho vya Miss Tabata 2011. Kushoto ni Mmoja wa washiriki wa Miss Chang'ombe ambaye hakika ni fimbo ya ukweli.
 Mwana dada Aisha Ramadhani "Aisha Mashauzi" aliwashika vilivyo na walikatika nyonga ile mbaya kwa taarabu yake kali.

Wadau mbalimbali wa Burudani na Urembo walihudhuria katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na Show kali kutoka kwao Twanga Pepeta “Kisima cha Burudani” na Mashauzi Clasic Modern Taarab kutoka kwake Mtoto wa Kikurya Aisha Ramadhani  ‘Mashauzi’.

Saturday, April 7, 2012

KANUMBA AACHA HAZUNI ,VILIO NA MAJONZI MAKUBWA KWA WATANZANIA NAMASHABIKI WAKE

HIVI NDIVYO ILIVYO KATIKA MSIBA WA STEVIN KANUMBA JIJINI DAR ES SALAAMMsanii wa maigizo nchini Dr Chen (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya michango ya msiba huo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
Pichani juu ni badhii ya mashabiki wa Kanumba waliopoteza fahamu na kudondoka chini baada ya kupata taarifa za kifo chake cha ghafla.
Miss Tanzania Happiness Magesa akimtuliza mmoja wa waombolezaji.
Umati wa waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Kanumba.
Mbuge wa Ubungo John Mnyika (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo, (Kulia) ni  ndugu Abdallah Mrisho.
Diwani wa Sinza Mr Simple (Kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Ubungo Mh: John Mnyika.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds FM, Ruge Mtahaba (aliyesimama) akimsikiliza Mhe:John Mnyika Mnyika.
Waombolezaji mbalimbali wakifarijiana kuhusu msiba wa kushitua wa Kanumba.
Msanii mahiri wa fialmu nchini tanzania Steven Kanumba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusukumwa na mpenzi wake wakiwa nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam. Mpenzi anayedaiwa kuwa nae amefahamika kwa jina la Lulu. Nyumbani kwa Marehemu Kanumba kumefurika waombolezaji wengi sana ambao wamefika kuomboleza msiba huo huku wengine wakija kuhakikisha kama habari ni za kweli.
(PICHA: Imelda Mtema, Erick Everist, Issa Mnally/GPL)

Monday, March 19, 2012

LOVE BETWEEN BLUE AND WAHIDA



BLU, WAHIDA PENZI MIAKA 7

                 Herry Samir ‘Blu’.
             Wahida.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Herry Samir ‘Blu’ amefunguka kuwa amekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi na demu aliyemtaja kwa jina la Wahida kwa miaka saba hivyo hawezi kumuacha kamwe.
Akizungumza na Ijumaa juzikati Blu alisema, yeye na Wahida wametoka mbali na wamevumiliana kwa mengi hivyo kumuacha itakuwa ni kosa kubwa katika maisha yake.
Alisema walikuwa wakiendesha uhusiano wao kwa siri sana na ndiyo maana hawakuwa wamevishana pete lakini sana anaamini ni muda muafaka wa kufanya hivyo.
“Nampenda sana Wahida, ni msichana wa maisha yangu na siku si nyingi nitadhihirisha upendo wangu kwake kwa kumvisha pete ya uchumba,” alisema Blu.
Alipobanwa juu ya tetesi zilizozagaa kitaani kuwa ana kidemu kingine kinamzingua mbali na Wahida, Blu alisema hayo ni maneno ya watu tu licha ya kwamba kuna wengi wanamshobokea.

HII NDIO TANZANIA YA LEO

Irene Pancras Uwoya.

*Asema Ababuu kamponza, laiti angejua...
HUKU madai ya kubeba mimba nje ya ndoa yakisambaa mithili ya moto wa kifuu, nyota wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amelifungukia Ijumaa na kusema kuwa, anajuta kufahamiana na kijana anayeitwa Ababuu kwa kuwa ndiye chanzo cha yote yanayosemwa.
Uwoya aliyefunga ndoa na msukuma kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ juzikati alisema kitendo cha yeye kuwa na ukaribu na kijana huyo ndicho kilichowafanya wabaya wake waibue ishu ya kuwa ni mjamzito na mhusika si mwingine bali ni huyo Ababuu.
“Kwa kweli najuta kuwa karibu na Ababuu kwani wabaya wangu wameitumia fursa hiyo kuzusha maneno ambayo hayana msingi juu yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish, alidai amekuwa karibu na Ababuu kwa mambo ya kawaida tu, wala hawakuwa wapenzi kama wengi walivyovumisha.
“Wabaya wangu wameitumia fursa ya mimi kuwa karibu na Ababuu kunichafua na laiti ningejua ningeuepuka mapema ukaribu huo,” alisema.

Je, mimba anayo?
Kila alipokuwa akiulizwa kuhusu kubeba ujauzito, Uwoya amekuwa hatoi ushirikiano wa kutosha na hivi karibuni alipokutana na mwandishi wetu licha ya kitumbo chake kuonekana kimetuna alisema: “Wewe unanionaje kwani, nina mimba au sina? Kwa kifupi siwezi kubeba ujauzito nje ya ndoa.”
Katika siku za hivi karibuni, Uwoya amekumbwa na skendo ya kudaiwa kubeba ujauzito nje ya ndoa huku mhusika akitajwatajwa kwa jina la Ababuu ambaye ni mpenzi wa zamani wa msanii wa filamu, Jacqueline Wolper.
Hata hivyo, licha ya mashosti zake kutoa ushuhuda kuwa anavyoonekana ana kibendi, kila alipoulizwa amekuwa akichenga kuzungumzia ishu hiyo.







MASHINE YA KUSIMAMISHA MATITI DER ES SALAAM KUPIGWA MARUFUKU



SIKU chache baada ya Wachina  kudaiwa kuingiza Dar mashine ya kusimamisha matiti yaliyolala, serikali na mamlaka husika vimeingilia kati na kupiga marufuku matumizi yake, Ijumaa linakuhabarisha.
Mashine hiyo iliyoripotiwa kuwa inapatikana katika saluni iitwayo Blue Palace, iliyopo Sinza- Mapambano, jijini Dar es Salaam, imegeuka gumzo kwa wanawake huku baadhi ya watu wakidai kuwa ni bomu litakalolipuka wakati wowote na kusababisha janga la kitaifa.
KWA NINI WACHINA WAMEILETA BONGO?
Ilidaiwa kuwa kama ilivyo kwa bidhaa nyingine, Wachina wamekuwa wakihusishwa na uingizaji madawa ya kukuza matiti nchini, hivyo baada ya kuwaharibu wanawake vya kutosha, sasa wamewaletea mashine ya kuinua kiungo hicho cha mwili  ikiwa pia ni mradi wao wa kujiingizia mkwanja.

NI KARIBU SANA NA MOYO
“Kukuza makalio kulikuwa kunaogopesha lakini hili la matiti ni hatari zaidi, kwani katika matumizi, mashine yenyewe inakuwa karibu sana na moyo, lazima kutakuwa na madhara,” alisema mwanamke mmoja na kuongeza:
“Unajua maelezo aliyoyatoa Ciisy Pang (mtaalamu wa Kichina anayetoa huduma hiyo saluni hapo) yanaogopesha. Anasema siyo kwamba ukishapata huduma hiyo matiti yanasimama siku zote za maisha, bali baada ya muda yanatepweta ‘so’ unatakiwa ufanyiwe mara kwa mara, huoni kama hapo kuna namna?”

WENYEWE  HAWANA  MATITI WALA MAKALIO!
“Mimi hawa Wachina huwa wananishangaza sana, mara utasikia wana madawa ya kukuza makalio, mara matiti au kurudisha usichana na nguvu za kiume, mbona wao hawajifanyii? Utakuta ni vimbaumbau na kifuani hakuna kitu, sidhani kama hiyo mashine ni salama,” alisema mwanamke mwingine akionesha shaka kwa kifaa hicho:
Akaongeza: “Chondechonde akina dada, kabla hamjaanza kuifakamia huduma hiyo, ni vema mkajua madhara yake kiafya. Nina kumbukumbu mbaya ya yale madawa ya kuongeza makalio, baadhi ya watumiaji walijikuta, ama makalio yameongezeka bila uwiano au yamekua hadi kero, tusije tukawa tunanunua kifo kwa fedha zetu wenyewe.”

WAZIRI MPONDA ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum juu ya mashine hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda alipiga marufuku kifaa hicho kutumika katika kipindi ambacho ameshaagiza wataalamu kukifanyia utafiti ili kubaini madhara yake.
“Tayari suala hilo linafanyiwa utafiti kubaini madhara yanayoweza kumpata mtumiaji. Kwa hiyo huduma hiyo isitishwe haraka hadi wataalamu watakaposema kama kuna madhara au la,” Waziri Mponda aliliambia Ijumaa.

ATUMA WATAALAMU KUKAGUA SALUNI ZA DAR
Waziri huyo alisema katika zoezi hilo amewatuma wataalamu kukagua saluni za Dar ili kubaini kama mashine hizo zipo kwani zinaweza zikawa zinatumika kinyemela.

TFDA YASAMBAZA WAPELELEZI
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza alisema tayari wameshasambaza wapelelezi ili kubaini kama mashine hiyo kweli ipo nchini.
Alisema kuwa pia maafisa hao wa mamlamka hiyo watachunguza kama ni mashine au kifaa tiba. Lakini wakati hayo yakiendelea, watoaji wa huduma hiyo wasitishe mara moja matumizi yake hadi majibu kamili yatakapopatikana. 

TUJIKUMBUSHE
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Kichina, mashine hiyo ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila ‘saizi’ kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli maalum kulingana na ukubwa anaohitaji mteja.
Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambapo huchukua wiki tatu mpaka sita kutegemeana na aina ya mteja na juhudi zake.
“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja akifika, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer  za nywele.
“Baada ya kumlaza mteja kitandani, tunachukua kitu mfano wa bakuli mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” alikaririwa mtaalamu huyo wa Kichina.
Akaendelea: “Tunaiwasha mashine kwa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika.”