Irene Pancras Uwoya.
*Asema Ababuu kamponza, laiti angejua...
HUKU
madai ya kubeba mimba nje ya ndoa yakisambaa mithili ya moto wa kifuu,
nyota wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amelifungukia Ijumaa na
kusema kuwa, anajuta kufahamiana na kijana anayeitwa Ababuu kwa kuwa
ndiye chanzo cha yote yanayosemwa.
Uwoya aliyefunga ndoa na msukuma
kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ juzikati alisema kitendo cha
yeye kuwa na ukaribu na kijana huyo ndicho kilichowafanya wabaya wake
waibue ishu ya kuwa ni mjamzito na mhusika si mwingine bali ni huyo
Ababuu.
“Kwa kweli najuta kuwa karibu na Ababuu kwani wabaya wangu
wameitumia fursa hiyo kuzusha maneno ambayo hayana msingi juu yangu,”
alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye
Krish, alidai amekuwa karibu na Ababuu kwa mambo ya kawaida tu, wala
hawakuwa wapenzi kama wengi walivyovumisha.
“Wabaya wangu wameitumia
fursa ya mimi kuwa karibu na Ababuu kunichafua na laiti ningejua
ningeuepuka mapema ukaribu huo,” alisema.
Je, mimba anayo?
Kila
alipokuwa akiulizwa kuhusu kubeba ujauzito, Uwoya amekuwa hatoi
ushirikiano wa kutosha na hivi karibuni alipokutana na mwandishi wetu
licha ya kitumbo chake kuonekana kimetuna alisema: “Wewe unanionaje
kwani, nina mimba au sina? Kwa kifupi siwezi kubeba ujauzito nje ya
ndoa.”
Katika siku za hivi karibuni, Uwoya amekumbwa na skendo ya
kudaiwa kubeba ujauzito nje ya ndoa huku mhusika akitajwatajwa kwa jina
la Ababuu ambaye ni mpenzi wa zamani wa msanii wa filamu, Jacqueline
Wolper.
Hata hivyo, licha ya mashosti zake kutoa ushuhuda kuwa
anavyoonekana ana kibendi, kila alipoulizwa amekuwa akichenga
kuzungumzia ishu hiyo.
MASHINE YA KUSIMAMISHA MATITI DER ES SALAAM KUPIGWA MARUFUKU
SIKU chache baada ya Wachina
kudaiwa kuingiza Dar mashine ya kusimamisha matiti yaliyolala, serikali
na mamlaka husika vimeingilia kati na kupiga marufuku matumizi yake,
Ijumaa linakuhabarisha.
Mashine hiyo iliyoripotiwa kuwa inapatikana
katika saluni iitwayo Blue Palace, iliyopo Sinza- Mapambano, jijini Dar
es Salaam, imegeuka gumzo kwa wanawake huku baadhi ya watu wakidai kuwa
ni bomu litakalolipuka wakati wowote na kusababisha janga la kitaifa.
KWA NINI WACHINA WAMEILETA BONGO?
Ilidaiwa kuwa kama ilivyo kwa bidhaa nyingine, Wachina wamekuwa
wakihusishwa na uingizaji madawa ya kukuza matiti nchini, hivyo baada ya
kuwaharibu wanawake vya kutosha, sasa wamewaletea mashine ya kuinua
kiungo hicho cha mwili ikiwa pia ni mradi wao wa kujiingizia mkwanja.
NI KARIBU SANA NA MOYO
“Kukuza makalio kulikuwa kunaogopesha lakini hili la matiti ni hatari
zaidi, kwani katika matumizi, mashine yenyewe inakuwa karibu sana na
moyo, lazima kutakuwa na madhara,” alisema mwanamke mmoja na kuongeza:
“Unajua maelezo aliyoyatoa Ciisy Pang (mtaalamu wa Kichina anayetoa
huduma hiyo saluni hapo) yanaogopesha. Anasema siyo kwamba ukishapata
huduma hiyo matiti yanasimama siku zote za maisha, bali baada ya muda
yanatepweta ‘so’ unatakiwa ufanyiwe mara kwa mara, huoni kama hapo kuna
namna?”
WENYEWE HAWANA MATITI WALA MAKALIO!
“Mimi hawa
Wachina huwa wananishangaza sana, mara utasikia wana madawa ya kukuza
makalio, mara matiti au kurudisha usichana na nguvu za kiume, mbona wao
hawajifanyii? Utakuta ni vimbaumbau na kifuani hakuna kitu, sidhani kama
hiyo mashine ni salama,” alisema mwanamke mwingine akionesha shaka kwa
kifaa hicho:
Akaongeza: “Chondechonde akina dada, kabla hamjaanza
kuifakamia huduma hiyo, ni vema mkajua madhara yake kiafya. Nina
kumbukumbu mbaya ya yale madawa ya kuongeza makalio, baadhi ya watumiaji
walijikuta, ama makalio yameongezeka bila uwiano au yamekua hadi kero,
tusije tukawa tunanunua kifo kwa fedha zetu wenyewe.”
WAZIRI MPONDA ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum juu ya mashine hiyo,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda alipiga marufuku
kifaa hicho kutumika katika kipindi ambacho ameshaagiza wataalamu
kukifanyia utafiti ili kubaini madhara yake.
“Tayari suala hilo
linafanyiwa utafiti kubaini madhara yanayoweza kumpata mtumiaji. Kwa
hiyo huduma hiyo isitishwe haraka hadi wataalamu watakaposema kama kuna
madhara au la,” Waziri Mponda aliliambia Ijumaa.
ATUMA WATAALAMU KUKAGUA SALUNI ZA DAR
Waziri huyo alisema katika zoezi hilo amewatuma wataalamu kukagua
saluni za Dar ili kubaini kama mashine hizo zipo kwani zinaweza zikawa
zinatumika kinyemela.
TFDA YASAMBAZA WAPELELEZI
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza alisema tayari wameshasambaza
wapelelezi ili kubaini kama mashine hiyo kweli ipo nchini.
Alisema
kuwa pia maafisa hao wa mamlamka hiyo watachunguza kama ni mashine au
kifaa tiba. Lakini wakati hayo yakiendelea, watoaji wa huduma hiyo
wasitishe mara moja matumizi yake hadi majibu kamili yatakapopatikana.
TUJIKUMBUSHE
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Kichina, mashine hiyo ina uwezo wa
kusimamisha matiti ya kila ‘saizi’ kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli
maalum kulingana na ukubwa anaohitaji mteja.
Kazi kubwa ya mashine
hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambapo huchukua
wiki tatu mpaka sita kutegemeana na aina ya mteja na juhudi zake.
“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili,
mteja akifika, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama
zilivyo dryer za nywele.
“Baada ya kumlaza mteja kitandani,
tunachukua kitu mfano wa bakuli mbili kulingana na ukubwa wa matiti
yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” alikaririwa
mtaalamu huyo wa Kichina.
Akaendelea: “Tunaiwasha mashine kwa dakika
45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka
litakapokamilika.”
No comments:
Post a Comment