Habari
za kusikitisha zilizotua hivi punde, Kwa masikitiko makubwa
tunasikitika kukutaarifu kuwa msanii maarufu aliyejizolea umaarufu kwa
kibao chake cha 'Mi Mmasai Bwana' Abel Motika maarufu kwa jina la
kisanii "Mr Ebo" amefariki dunia mapema leo hii. Inaripotiwa kuwa kifo cha msanii huyo kimeachasimanzi kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanga kwa ujumla ambapo ndio mahali alipokulia na kufanya shughuli zake za kisanii. Msanii
huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu na kutibiwa katika
Hospital mbali mbali hapa nchini na nje ya nchi na baada ya hapo
aliamua kupata matibabu ya dawa za kienyeji akiwa nyumbani kwao
Arusha.
Msanii atakumbukwa kwa nyimbo kama 'Mi mmasai, Boda boda,
Bado, Njaa Inauma' na nyimbo nyingine kibao. Pia ni mmiliki wa Studio
ya kurekodia Muziki ya MOTIKA Records iliyopo Tanga. Marehemu ameacha
mjane na watoto. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen
Anaitwa Joseph Kashinye, Mgombea
ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga. “Ninashughulikia kupata
mtandao wa uhakika. Leo siku haitoisha, nitakuwa nimepata suluhu la
tatizo la Mtandao. Nitawaporomoshea kila kinachojiri huku. Asubuhi hii
nimebahatisha kuingiza picha hiyo kwa taabu, imenichukua saa mbili
kuingiza picha moja! Pichani Kashindye alikuwa akihutubia maelfu ya
wakazi wa Igunga katika uzinduzi wa kampeni
.
Mabango yenye ujumbe tofauti katika
mkutano wa CHADEMA jana
.
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad
Slaa akihutubia mjini Igunga jana katika uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi mdogo jimboni hapa.
Dr Slaaa alisema CCM hawana sababu ya
kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ile kwani kwa kipindi cha miaka 50
imeshindwa kumkomboa Mtanzania katika lindi la umaskini.
Aliongeza kuseam kuwa CCM
wanachokizinatia ni kutumia kila mbinu ili kushinda chaguzi na kushika
dola ikiwa hawana malengo na mikakati madhubuti ya kumkomboa Mtanzania.
Aliwaasa wana Igunga kumchagua Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye, ili
awe mwakilishi wao kwani ni mtu makini anaetoka katika chama makini.
Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe
akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika mkutano wa uzinduzi wa
kampeni za chaguzi mdogo jimboni la Igunga.
Mbowe alisema kuwa wana Igunga mungu
amewapa bahati kubwa ya ufaya uchaguzi muda ,fupi baada ya uchaguzi
mkuu. Hivyo waitumie bahati hiyo wa kufanya mabadiliko.
CCM haistaili kurudishwa tena madarakani
jimboi hapa, kwani kuna masuala mengi ya msingi yanayohusiana na
maendeleo ya wananchi CC imeshindwa kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka
50
Ilifika zamu ya Mgombea wa Ubunge
jimboni hapa kwa Tiketi ya Chadema, Mwalimu, Mkaguzi wa Elimu, Joseph
Lashindye.Kashindye alisema kuwa wana Igunga wtarajie mabadiliko ya
haraka katika maendeleo.
Yeye ameamua kwa makusudi kuacha ualimu
na kuingia katika ulingO wa siasa. Amefanya kama Mwalimu Nyerere
alivyofanya kwani Mwalimu Nyerere, aliaacha ualimu na kujiunga na TANU,
matokea ya uamuzi huo wa mwalimu hakuna Mtanzania asiyeyaju.
Na yeye alisema kuwa endapo wana-Igunga
watamapa ridhaa ya kuwa mwakilishi atasimamia kwa nguvu zake zote
misingi ya utu, uchapakazi na atahakikisha anaziba mianya yote ya rushwa
katika halmashauri ya wilaya, ili fedha zinazotafunwa na wajanja,
zifanye kazi iliyokusudiwa ya kuwaletea maendeleo wana- Igunga.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John
Mnyika akiwahutubia wananchi wa jimbo la Igunga jana jioni
katikauzinduzi wa kampeni za ubunge jimboni humo.
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh.
Joseph Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.
Mbunge wa Mbeya Mjini-Chadema
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi aka Mr II(Sugu)akiwa amezungukiwa na
mashabiki wa chama hicho igunga muda mfupi baada ya Chadema kuzindua
Kampeni zake za Uchaguzi Mdogo.
Kutoka kulia ni katibu Mkuu wa
CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye mgombea ubunge wa Jimbo la
Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho na mbunge wa jimbo la Hai
wakielekea kwenye mkutano
.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika mkutano wa uzinduzi
wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la Igunga
.
Sehemu Kubwa ya Umati wa Wanachama
Wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)akielekea kwneye uzinduzi
rasmi wa kampeni za Kuwania jimbo hilo
Mabango yalikuwa ni mengi lakini
pia jeshi la polisi lilihakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha
KUSHINDWA KWA CHADEMA
IGUNGA KUNATUPATIA SOMO NA PICHA IPI?
UCHAGUZI mdogo wa Igunga umekwisha na
ktuachia mafunzo mengi. Kubwa kabisa ni kwamba, wananchi wanahitaji
mabadiliko kwa kila kitu katika maisha yao na kubwa zaidi linabakia kuwa
nani atakuwa kiongozi wa mabadiliko yao.
Dalili zote zinaonekana
zikielekea upande wa mabadiliko ya kweli japo pole pole na mabadiliko
haya siyo ya kichama ni ya watu binafsi mmoja mmoja, ni mabadiliko ya
fikra kwanza, kabla ya mabadiliko ya kura.
Hivi ni nani anaamini kuwa
leo hii jimbo kama la Igunga ambalo lilikuwa likiaminika kuwa ni ngome
tena ngome sugu ya CCM, leo wanavunja ngome yao na kukimbilia kambi ya
upinzani.
Kwa mtu wa kawaida na mwenye mawazo ya kawaida tu
lazima ajiulize kuwa je, hivi ni kweli kwamba mikutano ya kipindi
kisichozidi mwezi mmoja imewabadilisha kiasi hicho au ni mabadiliko
yaliyokuwamo ndani?
Mwingine atajiuliza swali, hivi yale maneno
yaliyokuwa yakivuma wakati fulani kuwa hiyo ni ngome ya chama tawala
yalikuwa ya kweli au yalikuwa ya kuokoteza tuu?
Ukifanya tathmini
kwa kina, utabaini kuwa kuna jambo linatokea kwa Watanzania ambalo ni
kukata tamaa kunakosababisha watu watake mabadiliko na mabadiliko
yamekosa mwongozaji na sasa wanaangukia kwa chama wanachodhani
kitawapeleka katika mabadiliko hayo.
Hakuna atakayaweza kuzuia
mabadiliko haya, siyo CCM wala serikali yake. Yawezekana CCM ndiyo ikawa
chanzo cha mabadiliko hayo au yawezekana pia Chadema au chama kingine
ikawa ndiyo kichocheo na kiongozi wa mabadiliko na haitashangaza.
Nimefuatilia
kwa makini matokeo ya uchaguzi ndogo wa Igunga wa Oktoba 2, CCM
kimeshinda kwa kura 26,484 huku Chadema kikivuna kura 23,260 kutokea
ziro ndani ya mwaka mmoja. Chadema kilishindwa kwa tofauti ya kura 3,224
huku kura 1,185 zikiharibika.
Kwa chama ambacho uchaguzi uliopita
kilikuwa hakishikiki Igunga, yaani CCM ambacho kilikuwa kikipita bila
ya kupingwa hii ni ishara ya kwanza kubwa ya upepo mbaya kuvuma kwao. Ni
kwamba bundi katua kwenye paa la nyumba yao!
Chadema
wameshindana na vikwazo vingi katika njia ya kufikia hapo ilipofika
ikiwamo kushindana na Serikali nzima, serikali ya wastaafu na vikosi vya
dola la taifa hili, ni ishara ya upepo wa mabadiliko kuvuma.
Hali
hiyo imeipa tabu sana CCM. Kutokana na wnanchi wa Igunga kukata tamaa
huko kumeibua chuki dhidi ya chama hicho na viongozi wake.
Ilikuwakabiliana na hilo chama kilikuwa kinatumia mtaji wa kuwatisha kwa
mbinu mbalimbali.
Kuna wakati watu walifikiria kwamba, Chadema
kingeshinda Igunga. Walifikiria kwamba , baada ya CCM kupoteza imani ya
wananchi wataendelea kuonyesha kinavyoporomoka baada ya kuondoka kwa
Rostam Aziz.
Kwa CCM kuachia au kupoteza ushindi upinzani wakati
wao kama chama, walitaka kuwaonyesha wananchi kwamba kuondoka kwa Rostam
si pigo la chama na chama kitaendelea kuwatumikia wananchi na si
Magamba.
Kwa muda wote CCM wamekuwa wakitumia vyombo vya dola
ambavyo wamerithi kutoka CCM ya chama kimoja toka wajumbe wa nyumba
kumi, wamekuwa wakitumia wajumbe wa Halmashauri za miji.
Wamewatumia
walimu na wakuu wa wilaya ili kuonyesha nguvu ya chama kiutawala, nguvu
ambayo vyama vya upinzani havina. Kwa kila hali, utaweza vipi
kushindana na chama kilichoshika mpini?.
Leo hii tunashuhudia
kinachotokea Igunga na kujifunza kumbe Chadema kina udhaifu katika
mkakati wa kuimarisha chama kwa maana ya kujenga mtandao. Mfano halisi
ni kwamba, chama hicho hakikuwapo kabisa kabla ya kuanza kampeni, lakini
kikawazoa wana-Igunga waliojikatia tamaa ndani ya wiki chache.
Ninavyoona
mimi Chadema kinapaswa kutumia vema umaarufu wake kwa watu kwa kujenga
mtandao, si kuishia kuruka kwa helikopta pekee wakati wa uchaguzi,
kubabaishwa na wingi wa watu kwenye mikutano yake na hatimaye kutokuwa
na uhakika wa kura kinazoweza kupata.
Kampeni za Chadema Igunga katika picha
Ummati ukiandamana kwenye kampeni za CHADEMA
Jimboni Igunga.
KAMPENI za kugombea ubunge Jimbo la Igunga zinaendelea huku vyama
vyenye upinzani mkali katika jimbo hilo vya CHADEMA, CCM na CUF
vikiendelea kunadi wagombea wao kwa mbwembwe.
Jimbo hilo limeachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa CCM Jimbo la Igunga,
Rostam aziz baada ya kujiuzulu kwa shinikizo kutoka ndani ya CCM.
Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionesha mikutano ya CHADEMA
Mikutano
ya CHADEMA Igunga
Kutoka kulia ni
katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye mgombea
ubunge wa Jimbo la Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho na
mbunge wa jimbo la Hai wakielekea kwenye mkutano
Mwenyekiti
wa Chama cha Chadema Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa kampeni katika
Kata ya Nkinga wa kuwania kiti cha Ubunge cha jimbo la Igunga baada ya
kuwasili na Helkopta
TAANZIA YA KIFO KWENYE
UCHAGUZI IGUNGA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya
Ubungo Mkoa wa Kichama wa Kinondoni Kanda Maalumu Dar es salaam
kinasikitika kutangaza kifo cha mwanachama Mbwana Masoud kilichotokea
wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
Marehemu Mbwana Masoud alikuwa ni mmoja wa wanachama walijitolea
kusafiri kwenda Igunga kwa ajili ya kuwa wakala kwenye uchaguzi
uliofanyika tarehe 2 Oktoba 2011. Marehemu Mbwana Masoud alitoweka
katika mazingira ya kutatanisha wilayani Igunga tarehe 2 Oktoba 2011.
Baada ya jitihada za viongozi wa chama kumtafuta marehemu
kushindikana Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika (Mb) alitoa taarifa polisi
tarehe 3 Oktoba 2011 na kufungua jalada RB/748/2011.
Tarehe 9 Oktoba 2011 wananchi wilayani Igunga walikuta mwili wa
marehemu ukiwa porini katika eneo ambalo linajulikana zaidi kama msitu
wa magereza. Taarifa ilitolewa na wananchi kwa diwani wa kata ya Igunga
Vicent Kamanga (CHADEMA) ambaye alifika katika eneo hilo na baadaye
maafisa wa polisi walifika na kupeleka mwili huo katika chumba cha
kuhifadhia maiti.
Tarehe 9 Oktoba 2011 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alitembelea
nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Kwa Jongo Kata ya Makurumla
kuifariji familia ya marehemu na kukubaliana na ndugu wa marehemu kutuma
wawakilishi wa chama na familia kwenda Igunga kuhakiki mwili
uliopatikana.
Tarehe 10 Oktoba 2011 wawakilishi wa familia wakiwa pamoja na Katibu
Mwenezi wa Chama Wilaya ya Ubungo Ali Makwilo walishuhudia mwili husika
na kuthibitisha kuwa ni wa marehemu Mbwana Masoud.
Leo Tarehe 11 Oktoba 2011 mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa
kidaktari (post mortem) kuweza kubaini chanzo cha kifo na ripoti
wamepatiwa jeshi la polisi. Hata hivyo, mazingira ya kupatikana kwa
mwili wa marehemu yanaashiria marehemu Mbwana Masoud aliuwawa.
Kutokana na hali ya mwili wa marehemu, maziko yatafanyika leo tarehe
11 Oktoba 2011 alasiri katika kata ya Igunga yakihusisha wawakilishi wa
familia ya marehemu, viongozi wa chama, wanachama na wananchi wa maeneo
husika kwa ujumla.
Viongozi waliopo kwenye maziko hayo ni pamoja na Katibu wa CHADEMA
Mkoa wa Tabora, Halfan Athumani, Diwani wa Kata ya Igunga Vicent
Kamanga na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga kupitia CHADEMA,
Joseph Kashindye.
Hitma ya Marehemu itafanyika hapa Dar es salaam nyumbani kwa marehemu
Mtaa wa kwa Jongo Kata ya Makurumla tarehe 13 Oktoba 2011 saa 7 mchana
baada ya swala ya adhuhuri na itahudhuriwa na viongozi waaandamizi wa
chama ngazi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
Chama kitaendelea kuwa pamoja kwa hali na mali na wafiwa katika
kipindi hiki kigumu na kinavitaka vyombo vya dola kuharakisha uchunguzi
ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wahusika. Marehemu amekufa
akiwa katika safari ya kulinda haki na kutetea demokrasia na maendeleo;
apumzike kwa amani.
MAUAJI YA KUSIKITISHA NA YA KINYAMA YANAYOTISHIA AMANI YA MTANZANIA
NI wakati wa kulaani siasa za
chuki na uhasama, kwani zimesababisha umwagaji damu maeneo mengi barani
Afrika na dunia kwa jumla, Tanzania mambo yameharibika na hivi ndivyo
wakala wa Chadema alivyouawa Igunga.
Masoud Mbwana, baba wa mtoto mmoja, hivi sasa amelala kwenye mwanandani
wa kaburi, chanzo kikidaiwa ni mchakato wa uchaguzi mdogo, uliochukuwa
nafasi Jimbo la Igunga Oktoba Pili, 2011
.
Mazishi ya Masoud Mbwana.
Mbwana, kada wa Chadema, alichukuliwa Dar es Salaam na chama chake
kwenda kusaidia shughuli za kampeni na uchaguzi, mwisho wa safari hiyo
ikawa ndiyo sababu ya kifo chake.
Wakala huyo, alikutwa ameuawa porini, macho yamenyofolewa na shingo
limevunjwa.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Ally Hassan Matumla, uchaguzi Igunga
ulifanyika Oktoba Pili, mwaka huu, siku iliyofuata walipokea taarifa
kutoka kwa vijana wengine wa Chadema kuwa Mbwana haonekani.
Katika mahojiano na mwandishi wetu yaliyofanyika Mtaa wa Jongo,
Makurumula, Magomeni, Dar, Matumla alisema kuwa kazi ya kumtafuta Mbwana
ilianza kufanywa na vijana wa Chadema ambao walikuwa wakiijulisha
familia hatua kwa hatua.
Mwili wa Masoud Mbwana ukiwa umetupwa porini. “Siku iliyofuata tukapewa taarifa kwamba kuna mtu amegongwa na
gari. Ikabidi familia initeue kwenda Igunga kufuatilia. Niliondoka Dar
Oktoba 6 na kufika Igunga siku hiyo hiyo saa 10:45 alasiri.
“Nilifika ofisi za Chadema, nikaongozana na viongozi hadi polisi. Hata
hivyo, yule aliyegongwa na gari hakuwa yeye. Jumapili (Oktoba 9), saa 8
mchana, tulipata taarifa kuwa kuna maiti ameokotwa porini, karibu na
Gereza la Igunga.
“Oktoba 10, tuliongozana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kwenda chumba
cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Wilaya ya Igunga, hapo ndipo
tulifanikiwa kumkuta akiwa na majeraha mengi.
“Mwili wa mdogo wangu ulikuwa na majeraha kisogoni, inaonekana
alipigwa, macho yalitobolewa, mikono na miguu ilikuwa na majeraha mengi
kuonesha aliburuzwa. Polisi walichukua maelezo yetu na kuuzika mwili
wake kwa sababu ulikuwa umeharibika mno,” alisema Matumla.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa amelaani mauaji hayo na
kuitaka serikali ifanye uchunguzi makini, kuwapata watuhumiwa.
Mwili wa Masoud baada ya kutolewa porini.
Slaa alisema: “Nawaomba wana familia muwe watulivu, ni msiba
mzito lakini tungoje uchunguzi utakaofanikisha kuwapata watuhumiwa.”
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
aliliambia gazeti hili kuwa chama chake kinalaani mauaji hayo, hivyo
kinawapa pole familia na Chadema kwa sababu Mbwana alikuwa wakala wa
chama hicho.
“Kwa kipindi hiki, tuache vyombo vya dola vifanye uchunguzi wake,”
alisema Nape.
Uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, ulitawaliwa na matukio mbalimbali ya
vurugu, ikiwemo nyumba kuchomwa moto, mwingine alimwagiwa tindikali na
mpaka risasi zilirindima katika vurugu za wafuasi wa CCM na Chadema.
Masoud Mbwana enzi za uhai wake.
Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea wa CCM, Dalaly Peter
Kafumu alishinda akifuatiwa kwa karibu na Joseph Kashindye wa Chadema.
BAADA YA MASOKO MAWILI KUUNGUA MBEYA, HAYA NDIYO YANAYOENDELEA
Watoto wakitafuta sarafu eneo lilipoungua soko la Sido Mwanjelwa Mbeya juzi.
Ujenzi ukiendelea eneo lilioungua soko la Sido Mwanjelwa Mbeya.
Baada ya kuunguliwa akina mama wanaendelea kujitafutua riziki pambeni kidogo mwa soko hilo
Chadema ilipotua eneo la ajali ya Mwanjelwa baada ya siku moja moto kuzimwa.
Hatimaye siasa zikandelea kata ya majengo Jijini Mbeya. PICHA KUTOKA MTANDAONI
Usiku
wa kuamkia leo huko jijini Mbeya,Moto ambao haukufahamika chanzo chake
uliteketeza soko dogo lililopo maeneo ya Forest ya zamani karibu na Chuo
kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu huria matawi ya Jijini Mbeya na
kusababisha mabada kadhaa kuteketea kwa moto ambao uliwahiwa na kikosi
cha zima moto cha mkoa wa Mbeya.
Mdau
alietuletea picha hizi ambaye alifika eneo la tukio mapema leo asubuhi
na kukuta moto umefanikiwa kuzimwa katika vibanda hivyo vilivyokuwepo
sokoni hapo na kutuletea taswira hizi za mabaki ya mabanda yaliyoungua
moto katika soko hilo yakiendelea kufuka moshi.
Mashuhuda
waliokuwepo maeneo ya jirani na soko hilo walisema Moto huo ulianza
majira ya saa 9:00 kamili usiku na muda si mrefu taarifa ziliwafikia
kikosi cha Zimamoto na wao walifika eneo la tukio dakika 10 baadae na
kufanikiwa kuuzima moto huo bila hata ya maigizo yao ya kila siku ya
kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji au kuharibika kwa gari wakati
wakiwa kwenye tukio.maswali
mengi sana yamekuwa yakiulizwa hivi sasa Jijini Mbeya juu ya majanga ya
moto katika masoko ya Mbeya kila siku na kwanini tahadhari
hazichukuliwi mapema na wakati hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa
mara??
USE YOUR PHONE IN PROPER WAY YOU'LL SEE IT'S IMPORTANCE
Habari zenyu
bana Mambo yanasemaje??
Hivi hasa kazi ya SIMU ni nini?
Hivi
kwani maisha bila SIMU hayawezi kwenda?
Kwani wazee wazamani walikuwa na SIMU? Lakini mbona waliishi.
Je unajua kwamba matatizo uliyonayo sasa moja
ya chanzo ni SIMU?
Umeshajipanga vipi kumaliza tatizo
hili la SIMU?
Imesha wahi kukutokea kama hii? (Ndiyo)
au ( Hapana)
Simu ni
kifaa muhimu sana katika maisha ya siku za lero, ila kinahitaji umakini mkubwa
kwani pindi unapokosea tu masharti yake hugeuka na kuwa kibaya kuliko hata SUMU.
Umuhimu
wa SIMU ni mkubwa hivi sasa kwasababu ya uwingi wa shughuli tunazokuwanazo. Kinacho
nichanganya na kunishangaza ni hikii, hivi binadamu anatakiwa kumiliki SIMU
akiwa na umri kuanzia miaka mingapi? Maana mimi nimewahi kushuhudia motto mmoja
chini ya miaka 10 akimiliki SIMU huku akidai kanunuliwa na mzazi wake. Hii kwangu
ilikuwa ni ajabu sijui kwako ? Je mzazi
huyu alikuwa sahihi kufanya hivyo kwa mototo wake? Je motto huyu anashughuli gain
zinazo mlazimu kununuliwa SIMU?. Je motto huyu anatumia SIMU hii kuwasiliana
na nani?
Ni dhahili
kabisa mototo huyu atapata tu watu wakuzunguza nao kwani watu wennye simu ni
wengi. Je hawa watu anaozungumza nao wote huzungumza lugha nzuri? Achana na
hayo, hayo 9, 10 ni hili, Je kuna yeyote anayefuatilia kuwa motto anaongea nini
na anaongea na nani?Hii ni hatari tena hatari kubwa.
Unapokuwa pekeyako
(yaani bila mke) simu huwa siyo tatizo kubwa. Ila sasa ukisha oa au kuolewa
SIMU linageuka kuwa tatizo na wakati mwingine una lazimika kupunguza au kufuta
kabisa baadhi ya mawasiliano ili kulinda na kudumisha heshima ya ndoa yenu. Ujue
kabla hujaoa au kuolewa niwengi walitaka na hata kulazimisha wawe wao lakini
ikashindikana, sasa watu kama hao mara nyingi
huendelea kukufuatilia lengo lao likiwa nikukuvuruga huku wakiamini kuwa ndoa
ikivunjika watapata wao nafasifi waliokua wameipoteza. Na kama hautakuwepo umakini basi dhamira yao
hutimia, kwani wapo wengi tu mtaani tunawaona.