Monday, March 19, 2012

HII NDIO TANZANIA YA LEO

Irene Pancras Uwoya.

*Asema Ababuu kamponza, laiti angejua...
HUKU madai ya kubeba mimba nje ya ndoa yakisambaa mithili ya moto wa kifuu, nyota wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amelifungukia Ijumaa na kusema kuwa, anajuta kufahamiana na kijana anayeitwa Ababuu kwa kuwa ndiye chanzo cha yote yanayosemwa.
Uwoya aliyefunga ndoa na msukuma kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ juzikati alisema kitendo cha yeye kuwa na ukaribu na kijana huyo ndicho kilichowafanya wabaya wake waibue ishu ya kuwa ni mjamzito na mhusika si mwingine bali ni huyo Ababuu.
“Kwa kweli najuta kuwa karibu na Ababuu kwani wabaya wangu wameitumia fursa hiyo kuzusha maneno ambayo hayana msingi juu yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish, alidai amekuwa karibu na Ababuu kwa mambo ya kawaida tu, wala hawakuwa wapenzi kama wengi walivyovumisha.
“Wabaya wangu wameitumia fursa ya mimi kuwa karibu na Ababuu kunichafua na laiti ningejua ningeuepuka mapema ukaribu huo,” alisema.

Je, mimba anayo?
Kila alipokuwa akiulizwa kuhusu kubeba ujauzito, Uwoya amekuwa hatoi ushirikiano wa kutosha na hivi karibuni alipokutana na mwandishi wetu licha ya kitumbo chake kuonekana kimetuna alisema: “Wewe unanionaje kwani, nina mimba au sina? Kwa kifupi siwezi kubeba ujauzito nje ya ndoa.”
Katika siku za hivi karibuni, Uwoya amekumbwa na skendo ya kudaiwa kubeba ujauzito nje ya ndoa huku mhusika akitajwatajwa kwa jina la Ababuu ambaye ni mpenzi wa zamani wa msanii wa filamu, Jacqueline Wolper.
Hata hivyo, licha ya mashosti zake kutoa ushuhuda kuwa anavyoonekana ana kibendi, kila alipoulizwa amekuwa akichenga kuzungumzia ishu hiyo.







MASHINE YA KUSIMAMISHA MATITI DER ES SALAAM KUPIGWA MARUFUKU



SIKU chache baada ya Wachina  kudaiwa kuingiza Dar mashine ya kusimamisha matiti yaliyolala, serikali na mamlaka husika vimeingilia kati na kupiga marufuku matumizi yake, Ijumaa linakuhabarisha.
Mashine hiyo iliyoripotiwa kuwa inapatikana katika saluni iitwayo Blue Palace, iliyopo Sinza- Mapambano, jijini Dar es Salaam, imegeuka gumzo kwa wanawake huku baadhi ya watu wakidai kuwa ni bomu litakalolipuka wakati wowote na kusababisha janga la kitaifa.
KWA NINI WACHINA WAMEILETA BONGO?
Ilidaiwa kuwa kama ilivyo kwa bidhaa nyingine, Wachina wamekuwa wakihusishwa na uingizaji madawa ya kukuza matiti nchini, hivyo baada ya kuwaharibu wanawake vya kutosha, sasa wamewaletea mashine ya kuinua kiungo hicho cha mwili  ikiwa pia ni mradi wao wa kujiingizia mkwanja.

NI KARIBU SANA NA MOYO
“Kukuza makalio kulikuwa kunaogopesha lakini hili la matiti ni hatari zaidi, kwani katika matumizi, mashine yenyewe inakuwa karibu sana na moyo, lazima kutakuwa na madhara,” alisema mwanamke mmoja na kuongeza:
“Unajua maelezo aliyoyatoa Ciisy Pang (mtaalamu wa Kichina anayetoa huduma hiyo saluni hapo) yanaogopesha. Anasema siyo kwamba ukishapata huduma hiyo matiti yanasimama siku zote za maisha, bali baada ya muda yanatepweta ‘so’ unatakiwa ufanyiwe mara kwa mara, huoni kama hapo kuna namna?”

WENYEWE  HAWANA  MATITI WALA MAKALIO!
“Mimi hawa Wachina huwa wananishangaza sana, mara utasikia wana madawa ya kukuza makalio, mara matiti au kurudisha usichana na nguvu za kiume, mbona wao hawajifanyii? Utakuta ni vimbaumbau na kifuani hakuna kitu, sidhani kama hiyo mashine ni salama,” alisema mwanamke mwingine akionesha shaka kwa kifaa hicho:
Akaongeza: “Chondechonde akina dada, kabla hamjaanza kuifakamia huduma hiyo, ni vema mkajua madhara yake kiafya. Nina kumbukumbu mbaya ya yale madawa ya kuongeza makalio, baadhi ya watumiaji walijikuta, ama makalio yameongezeka bila uwiano au yamekua hadi kero, tusije tukawa tunanunua kifo kwa fedha zetu wenyewe.”

WAZIRI MPONDA ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum juu ya mashine hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda alipiga marufuku kifaa hicho kutumika katika kipindi ambacho ameshaagiza wataalamu kukifanyia utafiti ili kubaini madhara yake.
“Tayari suala hilo linafanyiwa utafiti kubaini madhara yanayoweza kumpata mtumiaji. Kwa hiyo huduma hiyo isitishwe haraka hadi wataalamu watakaposema kama kuna madhara au la,” Waziri Mponda aliliambia Ijumaa.

ATUMA WATAALAMU KUKAGUA SALUNI ZA DAR
Waziri huyo alisema katika zoezi hilo amewatuma wataalamu kukagua saluni za Dar ili kubaini kama mashine hizo zipo kwani zinaweza zikawa zinatumika kinyemela.

TFDA YASAMBAZA WAPELELEZI
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza alisema tayari wameshasambaza wapelelezi ili kubaini kama mashine hiyo kweli ipo nchini.
Alisema kuwa pia maafisa hao wa mamlamka hiyo watachunguza kama ni mashine au kifaa tiba. Lakini wakati hayo yakiendelea, watoaji wa huduma hiyo wasitishe mara moja matumizi yake hadi majibu kamili yatakapopatikana. 

TUJIKUMBUSHE
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Kichina, mashine hiyo ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila ‘saizi’ kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli maalum kulingana na ukubwa anaohitaji mteja.
Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambapo huchukua wiki tatu mpaka sita kutegemeana na aina ya mteja na juhudi zake.
“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja akifika, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer  za nywele.
“Baada ya kumlaza mteja kitandani, tunachukua kitu mfano wa bakuli mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” alikaririwa mtaalamu huyo wa Kichina.
Akaendelea: “Tunaiwasha mashine kwa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika.”

No comments:

Post a Comment