SIMANZI YATAWALA KATIKA MAZISHI YA “THE GREAT STEVEN CHARLES KANUMBA.”
Mazishi ya aliyekuwa msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania Steven Charles Kanumba,
yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Steven Kanumba aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar
es Salaam, amezikwa na maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,
waliojitokeza kuaga mwili wake katika viwanja vya Leaders Club.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Waziri wa Habari, utamaduni, vijana na Michezo Dr. Emmanuel John Nchimbi amesema, “Tanzania imempoteza kijana shupavu aliyetumia vema kipaji chake kujitafutia maendeleo na pia kuitangaza nchi yake.“
Inasemekana zaidi ya Watu 200 walipoteza fahamu katika Mazishi yake, kutokana na watu wengi kuguswa sana na kifo chake, hasa wasanii wenzake wa Maigizo, na watu wa karibu yake.