Monday, March 19, 2012

LOVE BETWEEN BLUE AND WAHIDA



BLU, WAHIDA PENZI MIAKA 7

                 Herry Samir ‘Blu’.
             Wahida.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Herry Samir ‘Blu’ amefunguka kuwa amekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi na demu aliyemtaja kwa jina la Wahida kwa miaka saba hivyo hawezi kumuacha kamwe.
Akizungumza na Ijumaa juzikati Blu alisema, yeye na Wahida wametoka mbali na wamevumiliana kwa mengi hivyo kumuacha itakuwa ni kosa kubwa katika maisha yake.
Alisema walikuwa wakiendesha uhusiano wao kwa siri sana na ndiyo maana hawakuwa wamevishana pete lakini sana anaamini ni muda muafaka wa kufanya hivyo.
“Nampenda sana Wahida, ni msichana wa maisha yangu na siku si nyingi nitadhihirisha upendo wangu kwake kwa kumvisha pete ya uchumba,” alisema Blu.
Alipobanwa juu ya tetesi zilizozagaa kitaani kuwa ana kidemu kingine kinamzingua mbali na Wahida, Blu alisema hayo ni maneno ya watu tu licha ya kwamba kuna wengi wanamshobokea.

HII NDIO TANZANIA YA LEO

Irene Pancras Uwoya.

*Asema Ababuu kamponza, laiti angejua...
HUKU madai ya kubeba mimba nje ya ndoa yakisambaa mithili ya moto wa kifuu, nyota wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amelifungukia Ijumaa na kusema kuwa, anajuta kufahamiana na kijana anayeitwa Ababuu kwa kuwa ndiye chanzo cha yote yanayosemwa.
Uwoya aliyefunga ndoa na msukuma kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ juzikati alisema kitendo cha yeye kuwa na ukaribu na kijana huyo ndicho kilichowafanya wabaya wake waibue ishu ya kuwa ni mjamzito na mhusika si mwingine bali ni huyo Ababuu.
“Kwa kweli najuta kuwa karibu na Ababuu kwani wabaya wangu wameitumia fursa hiyo kuzusha maneno ambayo hayana msingi juu yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish, alidai amekuwa karibu na Ababuu kwa mambo ya kawaida tu, wala hawakuwa wapenzi kama wengi walivyovumisha.
“Wabaya wangu wameitumia fursa ya mimi kuwa karibu na Ababuu kunichafua na laiti ningejua ningeuepuka mapema ukaribu huo,” alisema.

Je, mimba anayo?
Kila alipokuwa akiulizwa kuhusu kubeba ujauzito, Uwoya amekuwa hatoi ushirikiano wa kutosha na hivi karibuni alipokutana na mwandishi wetu licha ya kitumbo chake kuonekana kimetuna alisema: “Wewe unanionaje kwani, nina mimba au sina? Kwa kifupi siwezi kubeba ujauzito nje ya ndoa.”
Katika siku za hivi karibuni, Uwoya amekumbwa na skendo ya kudaiwa kubeba ujauzito nje ya ndoa huku mhusika akitajwatajwa kwa jina la Ababuu ambaye ni mpenzi wa zamani wa msanii wa filamu, Jacqueline Wolper.
Hata hivyo, licha ya mashosti zake kutoa ushuhuda kuwa anavyoonekana ana kibendi, kila alipoulizwa amekuwa akichenga kuzungumzia ishu hiyo.







MASHINE YA KUSIMAMISHA MATITI DER ES SALAAM KUPIGWA MARUFUKU



SIKU chache baada ya Wachina  kudaiwa kuingiza Dar mashine ya kusimamisha matiti yaliyolala, serikali na mamlaka husika vimeingilia kati na kupiga marufuku matumizi yake, Ijumaa linakuhabarisha.
Mashine hiyo iliyoripotiwa kuwa inapatikana katika saluni iitwayo Blue Palace, iliyopo Sinza- Mapambano, jijini Dar es Salaam, imegeuka gumzo kwa wanawake huku baadhi ya watu wakidai kuwa ni bomu litakalolipuka wakati wowote na kusababisha janga la kitaifa.
KWA NINI WACHINA WAMEILETA BONGO?
Ilidaiwa kuwa kama ilivyo kwa bidhaa nyingine, Wachina wamekuwa wakihusishwa na uingizaji madawa ya kukuza matiti nchini, hivyo baada ya kuwaharibu wanawake vya kutosha, sasa wamewaletea mashine ya kuinua kiungo hicho cha mwili  ikiwa pia ni mradi wao wa kujiingizia mkwanja.

NI KARIBU SANA NA MOYO
“Kukuza makalio kulikuwa kunaogopesha lakini hili la matiti ni hatari zaidi, kwani katika matumizi, mashine yenyewe inakuwa karibu sana na moyo, lazima kutakuwa na madhara,” alisema mwanamke mmoja na kuongeza:
“Unajua maelezo aliyoyatoa Ciisy Pang (mtaalamu wa Kichina anayetoa huduma hiyo saluni hapo) yanaogopesha. Anasema siyo kwamba ukishapata huduma hiyo matiti yanasimama siku zote za maisha, bali baada ya muda yanatepweta ‘so’ unatakiwa ufanyiwe mara kwa mara, huoni kama hapo kuna namna?”

WENYEWE  HAWANA  MATITI WALA MAKALIO!
“Mimi hawa Wachina huwa wananishangaza sana, mara utasikia wana madawa ya kukuza makalio, mara matiti au kurudisha usichana na nguvu za kiume, mbona wao hawajifanyii? Utakuta ni vimbaumbau na kifuani hakuna kitu, sidhani kama hiyo mashine ni salama,” alisema mwanamke mwingine akionesha shaka kwa kifaa hicho:
Akaongeza: “Chondechonde akina dada, kabla hamjaanza kuifakamia huduma hiyo, ni vema mkajua madhara yake kiafya. Nina kumbukumbu mbaya ya yale madawa ya kuongeza makalio, baadhi ya watumiaji walijikuta, ama makalio yameongezeka bila uwiano au yamekua hadi kero, tusije tukawa tunanunua kifo kwa fedha zetu wenyewe.”

WAZIRI MPONDA ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum juu ya mashine hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda alipiga marufuku kifaa hicho kutumika katika kipindi ambacho ameshaagiza wataalamu kukifanyia utafiti ili kubaini madhara yake.
“Tayari suala hilo linafanyiwa utafiti kubaini madhara yanayoweza kumpata mtumiaji. Kwa hiyo huduma hiyo isitishwe haraka hadi wataalamu watakaposema kama kuna madhara au la,” Waziri Mponda aliliambia Ijumaa.

ATUMA WATAALAMU KUKAGUA SALUNI ZA DAR
Waziri huyo alisema katika zoezi hilo amewatuma wataalamu kukagua saluni za Dar ili kubaini kama mashine hizo zipo kwani zinaweza zikawa zinatumika kinyemela.

TFDA YASAMBAZA WAPELELEZI
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza alisema tayari wameshasambaza wapelelezi ili kubaini kama mashine hiyo kweli ipo nchini.
Alisema kuwa pia maafisa hao wa mamlamka hiyo watachunguza kama ni mashine au kifaa tiba. Lakini wakati hayo yakiendelea, watoaji wa huduma hiyo wasitishe mara moja matumizi yake hadi majibu kamili yatakapopatikana. 

TUJIKUMBUSHE
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Kichina, mashine hiyo ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila ‘saizi’ kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli maalum kulingana na ukubwa anaohitaji mteja.
Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambapo huchukua wiki tatu mpaka sita kutegemeana na aina ya mteja na juhudi zake.
“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja akifika, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer  za nywele.
“Baada ya kumlaza mteja kitandani, tunachukua kitu mfano wa bakuli mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” alikaririwa mtaalamu huyo wa Kichina.
Akaendelea: “Tunaiwasha mashine kwa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika.”

HOOOOOT NEWS



MAUAJI SONGEA YAMTIBULIA DIAMOND

Naseeb Abdul.
Na Herrsson Dawsson
TUKIO la vita na mauaji lilitokea wiki kadhaa zilizopita pande za Songea mkoani Ruvuma, limemtibulia ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul na kushindwa kufanya shoo pande hizo.
Akizungumza na Ijumaa baada ya kurejea jijini Dar es Salaam juzikati, akitokea mkoani humo, Diamond alisema alichukuliwa na promota aliyemtaja kwa jina moja la Eddo kwa ajili ya kwenda kufanya shoo katika Ukumbi wa Jambo Lee, Songea mjini, lakini ilishindikana kutokana na taarifa ya polisi kuwa hakuhitajiki mkusanyiko pande hizo.
“Nilifikia hotelini na kikosi changu cha kazi, niliambiwa maandalizi yamekamilika na tayari watu 800 walishakata tiketi, muda wa shoo ulipofika nilishangaa sipigiwi simu, ndipo nilimtafuta mhusika akaniambia imeshindikana kwa sababu za kiusalama ‘so’ nikapewa Sh. milioni moja nikarudi Dar na bado nadai Sh. milioni mbili.
“Kilichosababisha yote hayo ni mauaji yaliyotokea siku za nyuma na vita kati ya polisi na raia, lakini mashabiki wangu wasijali waendelee kunipigia kura ili nishinde Tuzo za Kili kwa kutuma neno Kili B1, Kili C2, Kili F3, Kili R1, Kili U1, Kili V3, Kili V4 kwenda namba 15747,” alisema Diamond.


Monday, March 19, 2012


HAPPY BIRTHDAY BONGO MOVIE CLUB

 Bongo Movie club yafanya party kubwa ya kutimizwa mwaka mmoja tangu ianzishwe iliyofanyika katika viwanja vya Bussiness iliopo maeneo ya Victoria. Ni vigumu sana kwa wasanii Tanzania kuanzisha kitu chenye umoja na kufikisha mwaka mmoja kwa kweli Bongo Movie club wanastahili sifa kubwa sana. maana kiuhalisia sisi wasanii bongo tuna matatizo sana atuna umoja wala upendo wa dhati toka katika mioyo yetu zaidi ya kuchekeana kichina tu lakini tunaamini kwa nguvu za Mungu wa imani tutabadilika na kuwa wenye upendo wa dhati.
 Viongozi wa Bongo Movie club wakipata picha ya pamoja The Greatest kati Richie Richie na Hartman Mbilinyi vijana wamendeza na suti zao za ukweli.

 Kama kawa mambo yakiwa yanazidi kunoga

 Wazee wa kale hao Mzee Korongo akiwa pamoja na mzee Mbembe kushoto party ilipendeza sana jamani

 Mnakumbuka jamani Bi Kidide enzi za Koale kukundi kilichotoa mastaa wengi mnaowaona sasa wakitesa katika tasnia za filamu 

 Wema Sepetu ndani ya Red Capet akipata interview toka kwa mtangazaji wa Staar tv Dada yetu Sauda Mwilima

 Wema na Ray

 Tino na Sandra

 Viongozi wakiteta jambo

 Wageni waliodhuria sherehe ya Bongo Movie club ya kutimiza mwaka mmoja

 Maya na Recheal picha ya kumbukumbu

 Wema sepetu na rafiki yake

 Johari na Uwoya

 Mwanamuziki wa kizazi kipya Sheta wa kati naye alikuwepo

 Steve Nyerere wa katikati pamoja Iddi aka( Mchongo) wa kulia

 Wolper na Odama kulia

 Amani kwenu warembo wa Bongo Movie club

 Rizi One Kikwete mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua rasmi party kwa kuwasha mishumaa kwenye keki rasmi iliyoandaliwa kwa siku hiyo
 Mwenyekiti wa Bongo Movie club JB akiweka mambo sawa katika upande wa keki

Keki yanye mfano wa Camera yani ikiashiria ndio kitendea kazi kukibwa sana katika upande wa kazi zetu, Bongo Movie club 2012 nitwaletea matukio mengine yaliyojiri mambo bado sana kulikuwa na burudani za kutosha

Wednesday, March 14, 2012


KONFA BUSINESS LODGE OPENING SOON

 Haya wadau wa town kuna kitu kipya kinakuja kuteka na kukamata jiji katika upande mzima wa sehemu ya  kupumzika kuna sehemu mpya inaitwa KONFA BUSINESS LODGE ni sehemu nzuri sana iko mitaa ya Mbezi Beach kwa maelekezo zaidi nitawafahamisha vizuri na inategemewa kufunguliwa wiki mbili zijazo ni sehemu nzuri sana na bei zao ni poa sana  karibuni sana
 Cheki geti ilo lakisasa kabisa wewe mwenyewe sema mimi sisemi

 RECEPTION

 Maandalizi yanaendeleaaa

 Chumba cha kulala

 Bafu, ni hatari sana jamani duhuuuuu



 Urembo wa kutosha ndani ya BUSINESS LODGE

 Simu ya chumbani ukitaka uduma

 Jamani hapa ni bongo wala si ulaya kila kitu sasa hivi kinapatikana bongo 

 Tv ya kuangalia baada mihangaiko ya mchana kutwa

 Mandhari ni nzuri sana jamani 

 The Greatest nikikagua baadhi ya maeneo

 Mambo yakiendelea

 Kiooo

 KONFA BUSINESS LODGE

 Kwa juu panavyoonekana

 Sehemu ya kupumzika ukiwa na mwenza wako

 KONFA BUSINESS LODGE

 Kiti cha massage

 Chumba cha nguvu

 Koridoni

 Geti

 Urembo wa kutosha maeneo ya BUSINESS LODGE

 WELCOME

 Bar

 Kwa nje panavyoonekana

 Mazingira safi sana

 Sehemu ya kupata moja baridi moja moto

Mzani wa kupima uzito baada ya kutoka msalani

Monday, March 12, 2012


PRINCIPLES NA SOBBING SOUND

 Wadau najua mmenituma kijana wenu mjini kuja kufanya kazi na si maneno mengi nami natekeleza maagizo yenu picha hizi nimepiga kwa ajili ya macover yangu mawili kwa ajili ya cinema zangu mbili kali zinazokuja nadhani itaanza Sobbing Sound imeshilikisha mastaa kibao wakali nitwaletea matukio ya mzigo huo ni hatari tupu
 Picha ya pamoja mimi na Uwoya huu sasa ni mzigo wa Sobbing Sound tumeunguluma pamoja humo ndani pata picha mwenyewe itakuwaje si ni hatari
 Lulu huu sasa ni mzigo wa Principles of Woman

 Pozi kama kawaida ya Lulu

 The Greatest na Uwoya

 Kissssssss

 Mtoto kakua jamani akiwa na Baba yake

 Hatari sana ndani ya Principles of Woman


 The Greatest

 Kijana kazini

 Handsome Boy