Monday, January 2, 2012

TUNATAKIWA KUWA WA ASILI KATIKA FILAMU ZETU

Tulianza kwa kuiga stori, sasa tunaiga majina ya filamu za Kiingereza, sijui baadaye tutaiga nini?


Tasnia ya filamu Bongo ambayo ipo katika nchi ya Waswahili wanaozungumza Kiswahili fasaha lakini inayoongoza kwa kuwa na majina mengi ya Kiingereza kwenye sinema zake! Bahati mbaya majina haya ya filamu tunayoyatumia tayari yameshatumika kwenye filamu za nchi zingine zilizoendelea zinazozungumza Kiingereza.

Filamu za Bongo nyingi zinaaminika kukopi hadithi na visa vya filamu zingine za nje, lakini hata hili la majina nalo limekuwa ni kitu cha kawaida jambo linalotuletea aibu kubwa miongoni mwa mataifa mengine. Hebu angalia mfano mdogo hapa chini:OFFSIDE  

What Is It?

Hizi ni baadhi ya filamu ambazo tumeiga majina...
 

No comments:

Post a Comment