MAFURIKO UWANJA WA NDEGE MWANZA YASABABISHA UWANJA KUFUNGWA KWA MUDA
Hali ilikuwa mbaya zaidi majira ya saa mbili asubuhi ambapo maji mengi yaliyokuwa yakitiririka kutoka eneo la mwinuko kaskazini mwa kiwanja cha ndege Mwanza, yalisababisha taswira ya uwanja kubadilika na kuwa kama sehemu ya mto mkubwa unaotiririsha maji kuelekea ziwa victoria.
Wafanyakazi mbalimbali kiwanjani hapo wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda eneo hilo.
Mafuriko yawatesa wakazi wa Kiseke, ilemela Mwanza
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwa wanahaha hapa na pale kutafuta kujikimu wakati wa mafuriko hayo
RC, RPC Dar watembelea eneo la mafuriko Sinza na Jangwani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadik Mecky Sadik, akionesha sehemu iliyoharibiwa na mafuriko, alipowatembelea wakazi wa Sinza kujua athari za mafuriko hayo Dar es Salaam. Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda.
y Kamanda wa Polisi Kanda Maaluma Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova, akionesha moja ya nyumba zilizoko ndani ya maji, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha Jijini leo. Watu watatu wamelipotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko hayo.
Watoto wanaoishi eneo la Jangwani wakiwa wamehifadhiwa kwenye kituo cha Daladala, kando ya Barabara ya Morogoro, baada kuzikimbia nyumba zao, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha Jijini Dar es Salaaam na kusababisha mafuriko
Wakazi wa Jiji wakiwa juu ya daraja la Jangwani, kukiangalia vitu mbalimbali vilivyosombwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko.
No comments:
Post a Comment