010
/
Posted by
KING HERRYSSON
DAWSSON

Mwanaume
wa nchini Marekani maarufu kama 'Half Man' ambaye maisha yake yote
amekuwa akiishi akiwa na nusu ya mwili wake tu kuanzia kiunoni ametamba
kuwa yeye ndiyo baba wa mtoto wa kike aliyezaliwa na mchumba wake ingawa
baadhi ya watu hawaamini kama kweli mtoto ni wake wakidai atakuwa
kabambikiwa mtoto.
Kenny Easterday mwanaume wa nchini Marekani mwenye
umri wa miaka 35 ambaye ana nusu mwili kuanzia kiunoni, anasubiria
majibu ya DNA ili kuwathibitishia watu kuwa yeye ndio baba wa mtoto wa
kike aliyezaliwa na mpenzi wake Nicky.
Katika documentary mpya
itakayorushwa hewani leo kwenye televisheni ya Marekani, Kenny mkazi wa
West Virginia anasema kuwa yeye ndiye baba wa mtoto Desiree aliyezaa na
mpenzi wake Nicky,33 miaka saba iliyopita.
"Watu wanataka kujua
kama Kenny ana sehemu za siri", alisema Nicky katika documentary hiyo
itakayorushwa hewani na televisheni ya The Learning Channel (TLC).
"Tunafanya mapenzi kama watu wengine, Kenny ana sehemu za siri kama mwanaume mwingine", aliongeza Nicky.
Kenny
alizaliwa akiwa na ugonjwa unaowapata watu wachache sana duniani
unaoitwa sacral agenesis ambao huzuia uti wa mgongo kukua kama kawaida.
Madaktari
walilazimika kuikata miguu yake miwili iliyojipinda iliyojichomoza
kidogo chini ya kiuno chake na kisha kuuchukua mfupa wa ugoko wake na
kuutumia kuurefusha uti wa mgongo wake.
Kenny ambaye kutembea kwake ni kwa kutumia mikono anasema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kupata mtoto.
"Nataka
niwe na mtoto atakayelibeba jina langu ambaye ataweza kusimama mbele ya
watu na kusema 'HUYU NDIYO BABA YANGU'", alisema Kenny.